Thursday, February 25, 2016

NYOTA WA BOLLYWOOD, SUNJAY DUTT, AACHILIWA HURU

Nyota wa filamu za Bollywood Sanjay Dutt amewachiliwa kutoka jela katika mji wa magharibi wa Pune nchini India.

Dutt mwenye umri wa miaka 56 alihukumiwa kifungo jela kufuatia makosa ya kumiliki silaha inayohusishwa na mlipuko wa 1993 mjini Mumbai ambapo takriban watu 257 waliuawa na wengine 713 kujeruhiwa.

Alipatikana na hatia ya kununua silaha hiyo kutoka kwa walipuaji ,lakini akasema kwamba silaha hizo zilikuwa muhimu kwa lengo la kuilinda familia yake wakati wa ghasia za Waislamu dhidi ya Hindu.

Nyota huyo baadaye alipelekwa hadi katika jela ya Pune mwaka 2013 ili kukamilisha kipindi chake cha miaka mitrano. Hatahivyo alipewa msahama wa siku 144 baada ya kuonekana kuwa na tabia njema na vitendo kama vile kusimamia kipindi cha redio. (BBC)


No comments:

Post a Comment