Imeripotiwa kuwa Bobby Brown anategemea kupata mtoto wa tatu na mkewe Alice Etheredge, ikiwa ni miezi saba baada ya kuzaliwa mwanae mwingine Bohdi. Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Bobby kumpoteza mwanae Bobbi Kristina (22) mwezi julai, 2015, ikiwa ni baada ya mtoto huyo kukutwa akiwa hajitambui bafuni, januari 2015 jambo lililosababisha kupoteza fahamu kwa zaidi ya miezi 6.
Bobby pia ni baba wa mtoto Cassius (6), LaPrincia(25) na Bobby Jr.(29) anayeishi London nchini Uingereza.
Pamoja na kwamba msanii huyo anafuraha isiyokifani kutokana na taarifa za ujauzito wa mkewe, inadaiwa kuwa Bobby Brown anapambana ili kuweka mambo sawa kutokana na kifo cha Bobbi Kristina.
Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo, chanzo kimoja kilitoa taarifa kuwa : “huu umekuwa mwaka mgumu kwa Bobby. Wakati mtu anapitia kipindi kigumu kiasi hiki, inakufanya uangalie na kujiuliza ‘nini kinaendelea?’
“baada ya kuzika mtoto, ni ngumu sana – sivyo inavyotakiwa kuwa. Kwa hali ya kawaida, anaendelea vizuri kama ilivyotarajiwa”
Bobby alimpongeza Alicia kwa ujasiri katika kipindi kigumu anachopitia miezi hii, alitoa pongezi hizo muda mchache baada ya kifo cha mwanae: “baada ya kumpoteza mama yangu, baba yangu, mke wangu, mtoto miaka sita iliyopita…kilichobakia ilikuwa ni kumtegemea Alicia.
“atakuwa ameshachoka mimi kuendelea kumtegemea, lakini hajanitupa na anaendelea kunibeba, na unajua kila nnapomuhitaji yupo kwaajili yangu”
No comments:
Post a Comment