Na Mwandishi Wetu
Kuzinduliwa kwa duka la kariakoo Airtel Xpress inaongeza idadi ya maduka kuongezeka kufatia uzinduzi wa dula jipya la kisasa lililoko Morocco Dar es salaam ulifanyika wiki iliyopita.
Katika uzinduzi wa duka la Airtel XPress kariakoo mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba alisema, kufunguliwa kwa duka la Airtel Xpress kariakoo itawawezesha wateja wa Airtel na wafanya biashara wa Kariakoo, Ilala, Magomeni kupata huduma zetu kwa ukaribu zaidi kama kujipatia simu za kisasa na kwa bei nafuu. Tunaimani kufunguliwa kwa duka hili hapa kutatasaidia kupata huduma kwa uharaka na ubora zaidi.
“Airtel tumejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu zaidi ya milioni 10 nchi nzima. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kiurahisi zaidi na kwa ufanisi wakati wote na hili limejidhihirisha leo kwa kufungua duka la Airtel Xpress”, aliongezea Adriana
Baadhi ya huduma zitakazotolewa kwenye duka la Kariakoo ni pamoja na Airtel Money, kusajili laini, huduma za internet na huduma zetu nyinginezo.
Pamoja na duka jipya lililozinduliwa kariakoo pia Airtel inamaduka sehemu mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam kama Airtel Morroco, Mlimani City, J Mall, Buguruni Airtel inatarajia kufungua maduka zaidi ifikapo Juni 2016 yatakayotoa huduma sambamba na mawakala wake Zaidi ya 80,000 nchi nzima.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam, akishuhudia ni wakala mkuu wa Airtel kutoka Celnet, Bwana Kalpesh Bandar
Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu simu mbalimbali za smartphone zinazopatikana katika duka jipya la Airtel Express Kariakoo wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Pichani ni Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati) akiwa na wateja pamoja na wafanyakazi wa Airtel
No comments:
Post a Comment