Tuesday, October 06, 2015

HATIMAYE VIJIJI VINNE WILAYANI HANANG’ VIMEPOKEA HATI ZA HAKIMILIKI ZA KIMILA ZA ARDHI‏‎.





   Mmoja kati ya wanakijiji waliopokea hati ya hakimiliki ya ardhi iliyotolewa Wilayani Hanang' na kudhaminiwa na shirika la Oxfam chini ya  shirika la Ujamaa Community Resource  Team(UCRT).



  Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel akizungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti.


 Baadhi ya wanakijiji wa Wilaya ya Hanang' waliohudhuria mkutano huo.


  Hawa ni mabinti wa kibarbaig waliokuwa kivutio kutokana na mavazi yao na moja kati ya waliotoa burudani na kufanya mkutano huo kuwa wa kipekee

 Wanakijiji wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa kutoa hati za hakimiliki za ardhi.


 Wananchi na viongozi wa Serikali ya kijiji  wakipitia kwa makini hati za hakimiliki za kimila za ardhi.


Sherehe zilipambwa na ngoma ya wa-Barbaig

 Hizi ndizo hati za haki miliki za ardhi zilizotolewa kwa vijiji vinne Wilayani Hanagh.




 Wananchi na viongozi wa Serikali ya kijiji  wakipitia kwa makini hati za hakimiliki za kimila za ardhi.

 Eveline Mirai, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' akizungumza na wananchi kuhusu kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali.





WENYEKITI wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi.

Zoezi hilo lilisimamiwa na kufadhiliwa na shirika la
Oxfam chini ya  shirika la Ujamaa Community Resource Team(UCRT).

Katibu tawala wa Wilaya ya  Hanang’John Gabriel,amekabidhi hati hizo akimuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya 100 kutoka katika vijiji hivyo ambavyo ni Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando.

Gabriel amesema hiyo itasaidia mtu kujua mipaka ya eneo lake hivyo hataweza kudhulumiwa ardhi kirahisi.

"Mara nyingi wakina mama ndio wanaothitika zaidi kwanihuwa wanakosa haki zao pale mume anapofariki, ananyanganywa mali zote ikiwa ni pamoja na ardhi wakati anaachiwa watoto awatunze,lakini wanapokuwa na hati za hakimiliki hakuna mtu anayeweza kuwapokonya kirahisi,"anasema.

Akizungumza kwa niaba ya wenyekiti wa vijiji hivyo,Mbisha Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi ameyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi na kuwasaidi kupata hati za hakimiliki za ardhi katika vijiji vyao.

"Sisi kama wafugaji hatukua tukijua thamani ya ardhi yetu lakini sasa tumeamka na tumejua haki zetu,manufaa na umuhimu wa kuwa na cheti cha umiliki wa ardhi"anasema Gicharoda.

Alisema vijiji vyao kupata hati za hakimiliki za ardhi itawasaidia kuwa na eneo la pamoja la malisho na kuwa na nguvu zaidi ya kuilinda ardhi yao na kuisimamia vyema hali ambayo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

Naye afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' Bi. Eveline Mirai ameshukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwasaidia wakina mama wajane kupata hati za hakimiliki za maeneo yao sambamba na kusaidia vijiji hivyo vinne kupata hati za vijiji.

Bi.Eveline amewataka wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwani mipaka hiyo imewekwa kwa gharama na wananchi wenyewe.

“Mtakapoheshimu mipaka hatutakua na migogoro ya ardhi tena na wananchi wenye maeneo yao wahakikisha wanapata hati za hakimiliki za maeneo yao ili wayamiliki kisheria,"anasisita.

Aidha meneja wa masuala ya ufugaji kutoka oxfam Laurent Wambura amesema serikali inatakiwa kushirikisha mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa ugawaji wa maeneo ya ardhi za vijiji ili kuongeza ufanisi katika sekta ya ardhi.


"Wanapogawa vijiji wakati bado mchakato wa upimaji unaendelea ni hasara kwa mashirika hayo kwani aidha yanalazimika kuanza kazi upya au kushindwa kwa sababu tayari fedha zinakuwa zimetumika na tatizo kwa wananchi linakuwa halijatatuliwa,"amesema Gabriel.


Akizungumzia changamoto amesema ni migogoro ya mipaka katika vijiji pamoja na udhaifu katika uongozi wa serikali ya vijiji ambazo huchelewesha mipango lakini pia kuchelewa kupata ripoti ya matumizi ya ardhi kutoka wizarani.


No comments:

Post a Comment