Wednesday, September 23, 2015

MKUTANO WA NNE WA BARA LA AFRIKA KUJADILI MIPANGO ENDELEVU NA MAFUNZO KWA VIJANA WAFANYIKA HOTELI YA GIRRAFE JIJINI DAR ES SALAAM.


 Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango na Maendeleo na Msimamizi wa Fedha na Uchumi wa Nchi za Maziwa Makuu, Rwanda, Burundi na Uganda, Br. John Njuguna akizungumza na wanahabari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Don Bosco.



 Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano



 Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwezeshaji akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Don Bosco.


CHUO cha Ufundi Stadi (VETA), kimesema kipo katika mchakato wa kuandika vitabu vya ufundi ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia nchini.

Hayo yamebainishwa na Mtunza Mitaala wa VETA, Rehema Binamungu katika Mkutano wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo.


Ambapo vitabu hivyo vitasaidia kutoa elimu ya ufundi katika vyuo vingine na shule mbalimbali nchini.
 

 Binamungu  amesema Veta inahitaji kuwa na vifaa vya ufundi vya kisasa ili kukabiliana na kukua kwa teknolojia ya ufundi ambayo inahitaji kuwa na vifaa hivyo ili kwenda sambamba na soko la ajira.

"Kutokana na kukua kwa teknolojia kwa sasa tunahitaji vifaa vya kisasa na maboresho ya vifaa ili twende sambamba na soko la ajira,"amesema Rehema.

Aliongeza changamoto nyingine inatokana na chuo hicho kutoa elimu ya ufundi kwa watu wenye elimu tofauti hivyo jitihada zinahitajika ili kutoa elimu bora,lakini piaVETA ipo katika mchakato wa kuandika vitabu vya kiufundi ambavyo vitasaidia kuinua elimu ya ufundi nchini"amesema Rehema.

Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana wanaopata mafunzo kwenye vyuo mbalimbali alisema ushirikiano unahitajika kati ya serikali na wadau mbalimbli ili kuhakikisha wanashirikiana kutoa elimu bora na yenye manufaa kwa jamii.

Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Don Bosco Afrika Mashariki, Padri Erick Mairura amesema mkutano huo utasaidia kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini .

Amesema hali ya kiuchumi kwa vijana bado ipo chini hivyo ni vyema serikali na wadau wa elimu ya ufundi wakashirikiana kuandaa maisha bora kwa vijana.

Amesema  mkutano huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini na utachangia kukuza ushirikiano kati ya sekta binafsi, wamiliki wa vyuo vya ufundi pamoja na serikali.

“Masomo ya ufundi yakitolewa ipasavyo yatasaidia kuwakwamua vijana katika changamoto mbalimbali hivyo ni muhimu sote tuone namna ya kuboresha vyuo vyetu na kuwawezesha vijana,anatoa wito pia Serikali kuviwezesha vyuo vya ufundi kwa kushirikiana navyo kwa karibu kama ambavyo nchi nyingine zinafanya,"anasema.


Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Ofsi ya Mipango na Maendeleo Afrika Magharibi- Don Bosco, Tsedi Yao Ati amesema kuwafundisha vijana ufundi kutasaidia kuboresha maisha yao kwani vijana wapo wengi na hawana shughuli maalum wanazozifanya kwa sababu mbalimbali.

Meneja Mradi wa Don Bosco, Badru Juma alisema wamekuwa wakishirikiana na makampuni mbalimbali katika kuwawezesha vijana kupata elimu mbalimbali kwa ajili ya kujikwamua.

Amesema barani Afrika kuna nchi 154 ambazo zina vituo vya Don Bosco na wamekuwa wakishirikiana katika kuondoa changamoto mbalimbali pamoja na kuwakwamua vijana ili waweze kujiajiri ama kuajiriwa.

“ Tumekuwa tukiangalia mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuwawezesha vijana na hivi sasa tumeanzisha utaratibu mpya wa kuboresha mahusiano kati yetu , sekta binafsi, VETA na serikali ili tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini,”amesema Juma.


No comments:

Post a Comment