Wednesday, August 26, 2015

MADAKTARI TOKA INDIA KUPAMBANA NA UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA KWA WATOTO

Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki. Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD baraniAfrika inaweza kuwa wengi sana.

Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa.  Baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu,  mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo,  kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. 

SOMA ZAIDI. . .

Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza  kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha
‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.

Watoto, hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni mgumu zaidi

Kutokana na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri, Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya  Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona  kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na mafanikio. 

Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto,  kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji unapochukua muda mrefu. 

Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.


No comments:

Post a Comment