Thursday, August 27, 2015

KAMPENI : MAGUFULI AINGIA MBEYA, APINGA SIASA ZA MAJI TAKA

Na Mwandishi Wetu Mbeya

Mgombea Urais wa CCM Dkt, John Magufuli amesema kuwa anakerwa mno na Siasa za kuchomeana moto Bendera za Vyama nakudai kuwa kufanya hivyo hakuwasaidia kitu. Dkt, Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Mbalizi lililopo Mbeya Vijijini Mkoa mpya wa Songwe

Alisema wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama vya siasa wamekuwa na tabia ya kuchomeana bendera zao moto jambo ambalo halileti maana yeyote. Amesema kuwa watu wanashindwa kuchapa kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo badala yake wanafanya mambo ya hovyo ambayo hayana tija.
SOMA ZAIDI . . .


"Ndugu zangu naombeni mnichague ili niwaletee maendeleo na nataka niwaambie kwamba katika kipindi chote cha uongozi wangu watanzania wajiandae kuchapa kazi tu hakuna mchezo wala mzaha. "anasema Dkt, Magufuli

Anasema kuwa hakuna maendeleo ambayo yanakuja kwa harakaharaka inachukua muda na lazima watu wafanye kazi na si kufikilia kuchomeana moto bendera.


No comments:

Post a Comment