Friday, July 17, 2015

SUNDAY OLISEH KOCHA MPYA WA SUPER EAGLES

Timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles imempa kibarua cha ukocha nahodha wake wa zamani Sunday Oliseh ( 40) (KUSHOTO).

Oliseh anachukua mikoba ya Stephen Okechukwu Keshi ambaye alitimuliwa mwanzoni mwa mwezi huu.

Kikosi hicho cha Oliseh kinatarajiwa kuja Tanzania mapema mwezi wa Septemba mwaka huu katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa afrika la mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment