Friday, July 17, 2015

MANGE KIMAMBI AWEKWA KIZUIZINI NA POLISI

Blogger, Mange Kimambi( Pichani Kulia), anadaiwa kuwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi baada ya kukamatwa na kuwekwa rumande muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalum jimbo la Ubungo, na kudaiwa kuwa muda wowote atapelekwa mahakamani.

Kupitia mitandao ya kijamii Mrekebishatabia ameandika “Habari nyingine, blogger maarufu Mange Kimambi amekamatwa na kupelekwa rumande. Watu walikua wakimfuatilia mpaka alipoenda kuchukua fomu ya kugombea viti maalumu jimbo la Ubungo ndipo akakamatwa, Anasubiri Kufikishwa Mahakamani Wakati Wowote. Tutajua zaidi kwanini amekamatwa!”

Kwa upande wa Lemutuz ameandika “Mange alipokwenda kuchukua fomu ya Ubunge WA Kinondoni akiwa na kaka yakeTawi L A CCM Mkwajuni Kinondoni.kumbe Nje kulikuwa na Polisi Mmoja wa Kiume na mwingine wa Kike waliokuwa wakimsubiri na Mtu mwingine anayedhaniwa kuwa ni kutoka Usalama wa Taifa…baada ya kumaliza kuchukua fomu tu akakutana na hawa watu 3 wakamuamuru aongoze Makao Makuu ya Polisi ambako alikaa kwa muda na kuelekea Polisi Osterbay ambako anashikiliwa mpaka sasa…TAYARI WATU WAWILI MAARUFU WAMESHAMFUNGULIA KESI MPAKA SASA SAA TANO KAMILI YA USIKU MWANAMKE MMOJA NA MWANAUME MMOJA MUME WA MTU MAARUFU SANA HAPA MJINI…pia juhudi za kumtoa kwa dhamana zinaendelea kwa nguvu kubwa sana…..BINAFSI BADO SINA LA KUSEMA HOWEVER SOON NITASEMA SOMETHING ABOUT THIS ISHU”

No comments:

Post a Comment