Thursday, July 23, 2015

NGOME YA MWISHO YA AL SHABAAB YATEKWA

Mji muhimu wa mwisho uliokuwa mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU) -miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya kwanza katika mji huo .

Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka usiku.

Vikosi vya AU nchini Somalia, na vile vya jeshi la Somalia, vilifanikiwa kuuteka mji huo baada ya mashambulizi makali. Majeshi kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia yamekua yakiendesha harakati za kuuteka mji wa Baadheere kwa siku chache zilizopita.

No comments:

Post a Comment