Wednesday, July 22, 2015

DAVIDO KUMFUATA ALI KIBA

Mwanamuziki nchini Nigeria, Davido (pichani kushoto) ambaye aling’ara sana nchini Tanzania, baada ya kufanya collabo na mwanamuziki Diamond, amefunguka kumfuata tena mwanamuziki mwingine baada ya kuvutiwa na wanamuziki wa nchini.

Akihojiwa wakati wa utoaji wa tuzo wa MTV MAMA, Davido, alidai kuwa Tanzania ni kama nyumbani kwake hivyo muda wowote ataachia ngoma na mwanamuziki Ali Kiba, baada ya kufanya collabo hata hivyo hakusema ngoma hiyo itatolewa na wapi, lini na kuwa itachukua muda gani kukamilika.

No comments:

Post a Comment