Monday, July 20, 2015

MABENKI YA UGIRIKI KUFUNGULIWA LEO BAADA YA KUFUNGWA KWA WIKI 3

Mstaafu akiwa amekaa kwenye benchi pembeni ya wateja waliojipanga mstari kuchukua fedha kwenye ATM nje ya benki ya taifa ya Ugiriki tawi la Thessaloniki
Hii leo mabenki ya Ugiriki yanatarajiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa wiki 3.

Mabenki hayo hata hivyo yanafunguliwa huku kkodi inayotozwa kwa bidhaa muhimu ikipandishwa ikiwemo pia kwa mahoteli na sekta nzima ya usafiri. hatua hii inanuiwa kurejesha imani a raia wa ndani ya Ugiriki na hata jamii ya kimataifa nje ya Ugiriki kufuatia msaada uliokuja kwa masharti ya kufanywa mageuzi kusainiwa wiki iliyopita na hivyo kukomboa nchi hiyo isifilisike.

Bado idadi ya juu zaidi ambayo raia wataruhusiwa kutoa kwenye akaunti zai itaendelea kudhibitiwa na benki kuu ya nchi. awali idadi hiyo iliwekwa kuwa Euro 60 kwa siku, japo sasa kuna matumaini idadi hiyo ikaongezwa hadi Euro 240 kwa siku. hata hivyo wengi wa raia wanasema kuwa kwa muda mrefu uchumi wa nchi hiyo umeharibika na wameshazoea kuishi kwa hata chini ya idadi hiyo kwa siku.

No comments:

Post a Comment