Thursday, July 30, 2015

BREAKING NEWS: MUDA WA KUJIANDIKISHA DAR WAONGEZW

Tume Taifa ua Uchaguzi(NEC) imeongeza siku nne zaidi kwa mkoa wa jiji la Dar es Salam kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura ili kuwezesha wakazi wengi kujiandikisha .

Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dares Salaam Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva (Pichani Kushoto) alisema uamuzi huo umetokana na kuwepo kwa mwamko mkubwa wa wananchi waliojitokeza kwa wingi isivyo kawaida katika vituo mbalimbali.

“Tume imeamua kuongeza musa wa kulizia watu watakaokuwapo vituoni siku ya mwisho yaani kesho tarehe 31,Julai, mwaka 2015. Sasa muda umeongezwakwa siku nne ili kumalizi unadikishaji huo,” alisema Jaji Lubuva.


Jaji aliongeza kwamba hivi sasa hadi kufikia jana tarehe 29 ,Julai wananchi waliojiandikisha katika daftari hilo ni 18,826,718 kwa nchi nzima , wakati lengo lilikuwa ni kufikia wananchi milioni 23 hadi 24.

Alisema hadi siku ya jana watu waliojiandikisha katika jiji hilo ni 1,754,725 sawa na asiliamia 62.4,wakati makadrio ni watu 2,810,423.


No comments:

Post a Comment