Serikali ya Afghanistan imeghadhabishwa na makubaliano ya Marekani kukubali kuwaachia huru wanamgambo watano wakuu wa Taliban, ili kuachiwa huru kwa mwanajeshi wa Marekani. Wafungwa hao kutoka gereza la Guantanamo walikabidhiwa Qatar.
Wengi walielezea ghadhabu kwa hatua hii. Kwa upande wa Afghanistan wanasema kuwa katika mpango kama huu, kwa mujibu wa sheria za kimataifa wafungwa hawastahili kukabisdiwa kwa nchi ya tatu. Lakini hilo sio sababu kubwa ya kuwatia matumbo joto.
Afghanistan hasira ya kubwa ni kuwa wafungwa wale wameachiliwa. Sasa wanawasiwasi kuwa mashambulio yatazidi. Watarudi kujiunga na kundi lao kwa maana kuwa serikali inajitahidi kupiga vita Al Qaeda ilhali Marekani inawaachilia, tena watano kwa ajili ya mwanajeshi wao mmoja.
Kwanza kabisa hao walioachiliwa sio wafungwa wa hivi hivi tu, ni mibabe walioshutumiwa kuwa miongoni mwa viongozi wa Al Qaeda. Kwa hiyo wadau wengi katika jamii yakimataifa wanahofia.
Bila shaka hii ni hatua kubwa nyuma katika kukabili Ugaidi na hasa Kundi hilo la AL Qaeda. Wadau wengi wana wasiwasi ni ujumbe gani hatua hii itatuma kwa magaidi wengine. Wafungwa sio hawa tu, Je Marekani itaendelea kufikia makubaliano na magaidi kama hawa ?
Taliban walimteka mwanajeshi mmoja wa Marekani (Bowe Bergdahl) ambaye inaaminika walimzuilia nchini Afghanistan kwa zaidi ya miaka 5.
Sasa wamekuwa wakidai kuwa wanataka viongozi wao waliokamatwa waachiliwe. Marekani imejaribu njia zote, na la kushangaza ni kuwa wamekiri wazi kuwa wameshindwa kumuokoa na ikabidi wafikie makubaliano na hao wanamgambo.
Sasa Bowe yupo hospitalini Ujerumani, anapokea matibabu na itachukua muda mrefu kabla ya kurudishwa nyumbani kwa wazazi wake, kwa kuwa ameathriika kisaikolojia na lazima kwanza atibiwe.
Chini ya sheria ya kimataifa hakuna ruhusa kwa yeyote kufanya mashauriano na watekaji nyara au hata kulipa ridhaa yoyote kwa watekaji nyara.
Kwa hiyo mashirika makubwa yakimataifa au hata nchi na serikali zinaposikia mfanyikazi wao ametekwa au mwnajeshi, kawaidia ni kutafuta mbinu za kumuokoa.
Huwa hawazungumzii kuwa wamelipa ili aachiliwe. Na japo kun abaadhi ya mashirika au nchi ambao wameshukiwa kulipa, hakuna anayekiri. Kukubali matakwa ya watekaji nyara ni kinyume na sheria za kimataifa.
Ni sababu hii imemfanya rais Barack Obama akemewe hata na wanasiasa kutoka nchini mwake hasa wa Republican. Japo wanasema kuwa wamefurahi mwanajeshi wao ameachiliwa, wengi wanashuku gharama iliyowafika ya kuwaachilia wafungwa watano wa Taliban. Tena viongozi. (BBC)
No comments:
Post a Comment