Sunday, June 01, 2014

MANJI KUIONGOZA KLABU YA YANGA KWA MWAKA MWINGINE MMOJA

Mfadhili na Mwenyekiti wa klabu ya Young African, watoto wa Jangwani jijini Dar es Salaam, Milionea Yusuf Mehbub Manji, ataendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja.

Katika mkutano mkuu wa klabu hiyo, wanachama wa Yanga waliokutana leo kwenye makao makuu ya ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyterbay jijini Dar es Salaam, wamefikia uamuzi huo.

Wanachama wa klabu hiyo, waliamua kumpa Manji miaka minane lakini yeye akakataa katakata na mwisho akakubali mwaka mmoja tu. Wanachama hao walikubali kwa kauli moja, bila hata ya mmoja kupinga katika kura za ndiyo zilizopigwa.

Mweyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga, Mama Karume alikuwepo na ndiye alianzisha hoja ya kutaka Manji aendelee kuiongoza Yanga kwa miaka mingine nane.


No comments:

Post a Comment