Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kimesonga mbele na
itakutana na Msumbiji katika hatua ya mwisho kuwania Kucheza makundi ya Kombe
la Mataifa Afrika nchini Morocco, mwakani.
Msumbiji imesonga mbele kwa kuwang'oa Sudan Kusini na sasa ni
zamu ya kuwavaa Stars. Stars imewang’oa Zimbabwe baada ya mechi iliyomalizika
hivi punde mjini Harare kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, Stars ilishinda
kwa bao 1-0 lililofungwa na John Bocco. Lakini katika mechi ya leo, kazi haikuwa
lelemama baada ya wenyeji Zimbabwe kupata bao mapema katika dakika ya 12
kupitia kwa Danny Phiri.
Lakini Stars chini ya Mart Nooij ikasawazisha katika dakika
ya dakika ya 26 kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’. Kipindi cha pili kiliponza
tu, Thomas Ulimwengu akaongeza la pili katika dakika ya 46 na dakika ya 55,
Willard Katsande akaisawazishia Zimbabwe.
Pamoja na juhudi za mwamuzi wa mchezo huo kuongeza dakika 7
za nyongeza, lakini bado mambo yalikuwa magumu kwa wenyeji na matokeo
hayakubadilika.
Hivyo Stars imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 na
inasubiri makundi sasa. Timu nyingine za Afirka Mashariki zimesonga mbele
ambazo ni Kenya, Uganda na Rwanda ambayo iliitungua Libya kwa mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment