Monday, May 05, 2014

BREAKING NEWS: MABOMU YALIPUKA NA KUUA KWENYE MABASI MAWILI MFULULIZO

Watu watatu wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa vibaya kutokana na mlipuko uliotokea katika mabasi mawili yaliyokuwa yamejaa abiria katika barabara ya Thika, jijini Nairobi. Mlipuko huo ulisababishwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu lililokuwa limewekwa katika mabasi yaliyokuwa yamebeba abiria jijini humo.

Polisi na baadhi ya mashuhuda walisema bomu lakwanza lililipuka jana saa 11 jioni karibu na eneo la Homeland ambapo bomu hilo lililipuka wakati basi linaelekea Githuri. Mlipuko huo ulisababisha hasara kubwa na kujeruhi vibaya waliokuwepo katika basi hilo la Jeean Sacco.

Kwa mujibu wa Standard Media ya Kenya, bomu la pili lililipuka dakika chache baadaye eneo la Roysambu na kusababisha watu wawili waliokuwa katika basi hilo kupoteza maisha. Basi hilo Mwiki Scco lilikuwa linasafirisha abiria 51 kutoka mjini wakati bomu hilo linalipuka.
Kwa mujibu wa polisi na baadhi ya mashuhuda, matukio hayo yalipangwa kwa hali ya juu sana. Msemaji wa Polisi Bi. Gatiria Mboroki alisema kuwa milipuko hiyo imesababishwa na vitu vinavyosadikiwa kuwa ni mabomu kutoka katika vitu vilivyokuwa vimeachwa katika mabasi hayo au kutegeshwa kwa makusudi.
“Tunachukua fursa hii kuwaomba waendesha matatu kuwachunguza abiria wao na mizigo yao kwa usalama wao. Matukio haya yangeweza kuepukika” alisema Mboroki


No comments:

Post a Comment