Utaona video chini jinsi tangazo hilo lilivyokuwa linatengenezwa, ambapo mpiga picha wa Kijapan, “Photographer Hal” akielezea jinsi alivyovutiwa na wazo hilo na jinsi alivyopiga picha hizo.
“Binadamu hawajakamilika kama wa pekeyao. Ni mpaka wanapokuwa pamoja, wanapokuwa wamekaribiana, ndio wanakuwa wamekamilika kabisa” anasema na kuendelea “na ndio maana nikawafungasha pamoja” wapenzi ambao wameingizwa katika mfuko mkubwa wa plastiki kwa sekunde 10 na kuvuta hewa ya oxygen kutoka katika kikopo wakati Hal anaendelea na zoezi hilo.
SHUKA CHINI UONE VIDEO JINSI TANGAZO HILI LINATENGENEZWA
No comments:
Post a Comment