Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa Mtayarishaji Filamu wa Bongo Movie, George Tyson amefariki dunia. Tyson amepoteza maisha baada ya kupata ajali huku akiwa na wenzie 8. Katika ajali hiyo inasemekana Tyson ndiye pekee aliyepoteza maisha.
Marehemu Geogre Tyson pichani alienda katika kijiji cha Chilonwa Chamwino kwaajili ya kutoa msaada wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Akiwa safarini kurejea jijini Dar es Salaam, mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka safari ya kurudi Dar es Salaam ianze, karibu na Gairo mjini, mkoani Dodoma.
Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika hospital ya Mkoa Morogoro, mpaka tunakwenda mitamboni safari ya kuuleta Dar es Salaam imeshaanza. Mwili wa Marehemu utaingia wakati wowote kuanzia sasa katika Hosptili ya Muhimbili kabla ya taratibu nyingine kuendelea.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
No comments:
Post a Comment