Friday, May 24, 2013

OBAMA ANAFUATANA NA WATU 700 KUJA TANZANIA


Rais wa Marekani, Barack Obama, atafuatana na kundi la watu 700 katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania inayotarajiwa julai mosi mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,


Bernard Membe, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

Membe aliwataka wafanyabiashara wenye hoteli, migahawa, magari ya kukodisha waboreshe biashara zao ili Wizara hiyo iingie mkataba nao. Akiwa nchini, Rais Obama atafanya mkutano na viongozi wa nchi zinazoendelea kwa kuzungumzia umuhimu wa sayansi na teknolojia katika nchi zao.

“Ugeni huu mkubwa, utaisaidia nchi kupata pesa za Miradi ya Changamoto za Milenia (MCC), ambazo zitatumika katika maji, elimu na barabara. Pia Rais Obama atazungumzia jinsi nchi za Afrika zitakavyopata umeme wa kutosha tofauti na sasa. Kimsingi tumejiandaa katika mapokezi yake hata kwenye mavazi,” alisema Membe.

Waziri Membe alisema tayari baadhi ya ujumbe ambao ataongozana nao umeanza kuwasili nchini kwa matayarisho.

No comments:

Post a Comment