Tangazo la chuo hicho kilichoko Boston, Marekani lililotolewa ijumaa iliyopita, limesema kuwa aliyekuwa kocha na meneja wa timu ya Manchester United amekubali kuchukua kazi ya kufundisha katika programu mpya inayoitwa “Business Entertainment, Media and Sport(Biashara, Burudani, Habari na Michezo)”
Ferguson alistaafu mwezi may, 2013 akiwa ameipatia timu yake makombe 13, kombe lake la 49katika Ligi mbalimbali baada ya kufundisha kwa zaidi ya miaka 39 kama meneja kwenye soka.
Ferguson mwenye miaka 72 ameshawahi kufundisha Harvard, lakini ameamua kuchukua hiyo nafasi ambapo atafundisha kuanzia mwezi ujao. “Nina furaha sana kupata fursa na nafasi ya kuchangia katika kituo cha ubora” Ferguson alisema katika taarifa iliyotolewa na chuo hicho.
“Muda ambao tayari nilishafundisha Harvad umekuwa ni muda wa hamasa ya uzoefu na natumaini ntaendeleza kwa vitendo mahusiano na wanafunzi, kitengo na marafiki wa Jamii ya Shule ya Biashara ya Harvad”
Ferguson ameshawahi kushiriki katika madarasa kadhaa HBS akishirikiana na Profesa Anita Elberse na ameshirikiana naye katika kuchambua mbinu mbalimbali za utawala.
“Tuna hamu kubwa na tunamkaribisha Sir Alex Ferguson hapa kampasi ya HBS kuchangia katika safari yake ya uongozi, na kuchangia katika elimu ya juu na kuweza kuleta mabadiliko makubwa dunuani.” Alisema Elberse
TAFADHALI TOA MAONI YAKO HAPO CHINI

No comments:
Post a Comment