Wanawake hao walitambulishwa kwa mchungaji huyo mwaka jana mwezi disemba ambaye aliwaahidi kuondoa mashetani yaliyowasumbua kwa muda mrefu, na wamekuwa wakifuatilia maombi yake toka wakati huo kwaajili ya kusafisha nyoyo zao.
Wanawake hao mwishoni mwa wiki waliugua na kupelekwa hospitali ambapo daktari aliwafanyia vipimo na kugundua kuwa wote wawili ni wajawazito. Mama alikiri kuwa ni ujauzito wa mchungaji baada ya kutembea naye.
Mama huyo aliamini kuwa mtoto wake ana mpenzi wa siri na kumtaka amtaje, lakini msichana huyo alimtaja mchungaji Sam. Familia hiyo sasa hivi imechanganyikiwa.
Ilitambulika kuwa mwanamke huyo na mwanae walikuwa na mashetani baada ya mumewe kufariki kwa kuumwa ugonjwa wa ajabu wa tumbo, ambapo wazee wa kijiji walitafuta tiba kwa waganga ambao walidai kuwa mwanamke huyo na mwanae wanahusika na ugionjwa wa baba huyo.
Mchungaji Sam, amewapa mimba mama mwenye umri wa miaka 45 na mwanae (14) kwa madai kuwa alikuwa katika maombi uya kuondoa mashetani waliyokuwa wakipambana nayo.
Taarifa za mimba zilipotoka, mchungaji huyo aliyehisi kuna tatizo, alitoweka kusikojulikana na kuliacha kanisa ambalo amekuwa akiliongoza huku akiwa anawafanyia maombi maalumu wanawake ndani ya chumba ambacho hufunga kwa ufunguo.
Akidhibitisha taarifa za ujauzito, dada mkubwa wa mwanamke huyo, Elizabeth Agu alisema “tumejaribu kumtafuta mchungaje wanayedai ndio muhusika wa mimba hizo kwa kutumia simu lakini simu hiyo imezimwa na hajulikani mahali alipo, na kanisa limefungwa makufuli”
No comments:
Post a Comment