Brazil ilichaguliwa bila kupingwa mwaka 2007 baada ya shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kuamua kuwa mashindano hayo yatafanyika Amerika ya Kusini kwa mara ya kwanza toka mwaka 1978 huko Argentina, na hiyo itakuwa ni mara ya tano kwa ujumla kufanyika Amerika Kusini.
Timu za mataifa 31 zimefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho, mchakato ambao ulianza kutafuta watakao fuzu mwaka 2011. Kutakuwa na jumla ya mechi 64 katika miji 12 nchini Brazil katika aidha viwanja vipya kabisa au vilivyokarabatiwa, ambapo mpambano utaanza kwa makundi.
Kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia, mechi zitachezwa huku teknolojia mpya ijulikanayo kama Goal-Line itatumika. Pamoja na mwenyeji wa kombe hilo, Brazil, washindi (Uruguay, Italy, Germany, England, Argentina, France and Spain) wa kombe hilo miaka iliyopita toka kuanzishwa mwaka 1930 pia wamefuzu kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Spain ndio bingwa mtetezi wa mashindano hayo, baada ya kuibuka mshindi kwa kuichapa Uholanzi 1-0 katika Kombe la Dunia la mwaka 2010 na kuwa ndio mara yao ya kwanza kutwaa ubingwa katika historia ya kombe la dunia.
Mara nne za mwisho mashindano hayo kufanyika Amerika ya Kusini, Kombe hilo lilifanikiwa kubaki katika timu za bara hilo.
No comments:
Post a Comment