DAVID MOYES, Meneja wa Machester United aliyechukua mikoba toka kwa Sir Alex Ferguson, akiwa na furaha kama anavyoonekana katika picha hapo juu baada ya kuambiwa atalipwa kitita cha pauni milioni 38 akifukuzwa Manchester United.
Meneja wa klabu ya Manchester United, David Moyes yuko mbioni kufukuzwa na wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer kutokana na matokeo mabovu aliyoonesha katika msimu wa ligi akiwa katika klabu hiyo ya Old Trafford.
Ikiwa ni miezi 11 toka asaini mkataba wa miaka 6 wa kuendesha klabu hiyo akiwa ni chaguo la Meneja aliyeondoka Sir Alex Ferguson ili kushika nafasi yake. Inadaiwa Moyes amepoteza kuungwa mkono na familia ya Glazers pamoja na viongozi wa klabu hiyo, baada ya timu hiyo kuchapwa bao 2-0 na Everton.
Imedaiwa kuwa endapo Moyes ataondoka Old Trafford atalipwa kwa kuvunjiwa mkataba wake kitita kisichopungua pauni za Uingereza milioni 38 (shilingi za kitanzania 104,353,700,000)
Mwisho wa Moyes, 50, kuwa katika klabu hiyo unaweza usifikie mwisho wa wiki akiwa Old Trafford ambapo timu hiyo itakutana na Norwich City, endapo atashindwa kudhibitisha uwezo wake basi siku zake katika klabu hiyo ziko mwishoni, wakati inadaiwa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward hana dalili za kuendelea naye.
Wafanyakazi wanaomsaidia Moyes waliochukua nafasi za makocha wa Ferguson kama Mike Phelan na Rene Meulensteen inadaiwa pia wako njia panda, kundi hilo ni pamoja na Steve Round, Jimmy Lumsden na Phil Neville, waliojitahidi kujitengenezea heshima kwa kuwasaidia wachezaji.
TAFADHALI TUPIA MAONI YAKO HAPA CHINI. . .
No comments:
Post a Comment