Mtoto wa miezi 9 amefikishwa mahakamani kwa kudaiwa
kushiriki kupanga mauaji. Mtoto huyo Muhammad Mosa Khan(Pichani Kushoto), pia anashtakiwa kwa
kutishia polisi na kuingilia masuala ya taifa. Pia mtoto huyo anashtakiwa pamoja na wengine kwenye familia
yao baada ya kuvamiwa na polisi na kukamatwa mtuhumiwa wa wizi wa gesi jijini
Lahore.
Kwa mujibu wa gazeti la Express Tribune, mtuhumiwa aliachiwa
kwa dhamana baada ya kufikishwa mbele ya mahakama chini ya Jaji Rafaqat Ali
ambapo alifika na babu yake, Muhammad Yassen.
Hata hivyo kichanga hicho kilianza kulia mahakamani baada ya
babu yake kumchovya dole gumba lake kwenye wino na kuweka kwenye hati ya
dhamana, kwani mtoto huyo hawezi kuweka saini mwenyewe.
ENDELEA KUSOMA. . .
Wakati kichanga hicho kinashtakiwa rasmi alhamisi iliyopita,
alikuwa ananyonya chupa yake ya maziwa, kwa mujibu wa gazeti la Express Tribune. Mtoto huyo akiwa na babu yake na wajomba zake,
walimshambulia ofisa wa polisi, walinzi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya
gesi ya SUI kwa kutumia vyuma na mawe.
Tukio hilo lilitokea wakati timu ya polisi na walinzi na baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni ya Sui, walivamia mtaa wa Muhalla Thanedaran kwaajili
ya kukata gesi kwenye nyumba ambazo hazijalipia bili zao na zina madeni.
Polisi walitoa malalamiko dhidi ya familia nzima lakini
hawakujisumbua kuangalia kwamba kuna mtoto mmoja tu, mwenye umri wa miezi 9,
ambaye Yaseen alimleta mahakamani katika kesi hiyo.
Inspekta msaidizi, Kashif Ahmed anadaiwa kusimamishwa
kazi kwa kufungua kesi dhidi ya mtoto.
No comments:
Post a Comment