Iringa
Waziri Mkuu mstafu Edward Lowasa ametoa msaada wa
chakula kwa ajili ya kumaliza arobaini ya aliyekuwa shekhe Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Marehemu Alhaji Ali Juma Tagalile iliyofanyika juzi Nyumbani kwake mjini
Iringa.
Shekhe Tagalile alifariki dunia Machi 6 mwaka huu katika
hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa alikokuwa amelezwa kufuatia kusumbuliwa na
ugonjwa wa shinikizo la damu. Lowasa ambaye hakuhudhuria hitima hiyo iliyoambatana na
kusomwa kwa dua alitoa msaada wa vyakula kupitia kwa mwakilishi wake Fadhili
Ngajilo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Ngajilo ambaye ni
mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa
alisema Lowasa ametoa msaada huo kutokana na mahusiano mazuri aliyokuwa nayo na
marehemu wakati wa uhai wake.
“Mh.Lowasa alisema ameamua kutoa msaada huu kama sehemu yake
ya kumlilia Marehemu Tagalile kutokana na uhusiano mzuri waliokuwa nao wakati
wa uhai wake,alifanya nae kazi vizuri na pia alikuwa mshauri kwa mambo
mengi”alisema Ngajilo.
Akitoa shukurani zake kwa tukio hilo msemaji wa familia ya
Marehemu, Said Tagalile ambaye pia ni mdogo wa marehemu alimshukuru mh. Lowasa
kwa msaada wake na kuongeza kuwa umesaidia kufanikisha shughuli hiyo muhimu.
“Sisi kama wanafamilia tumefarijika na sadaka
hii,tunawashukuru watu wote waliojitokeza kutufariji na pia tunamshukuru Lowasa
kwa kutupatia sadaka iliyofanikisha zoezi hilo muhimu tunamuombea kwa mungu
pale alipopunguza mwenyezi mungu amuongezee"alisema Tagalile.
Said alitaja vitu vilivyotolewa na Lowasa kwa ajili ya
kuhitimisha arobaini ya Shekhe huyo ambaye ni kaka yake kuwa ni Gunia nne
za Mchele,Ng’ombe mmoja na Ndoo mbili za mafuta ya kula zenye ujazo wa
lita 20 vyote vinadaiwa kugharimu kiasi cha Sh milion 1.5
Marehemu ambaye katika kipindi cha uhai wake alikuwa shekhe
Mkuu wa mkoa wa Iringa pia amewahi kujishughulisha na mambo mbalimbali ya
kijamii kiuchumi na kisiasa.
Said alitaja baadhi ya nyazifa alizoshika marehemu Tagalile
wakati wa uhai wake kuwa ni pamoja na wenyekiti wa Bodi ya Msamaha wa Wafungwa
Mkoa wa Iringa (Parole)Daktari wa magonjwa ya binadamu tangu enzi ya mkoloni na
pia mshauri wa masuala ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment