Saturday, April 12, 2014

BUSINESS TIMES LIMITED YATWAA UBINGWA MICHEZO YOTE YA NSSF

Timu ya mpira wa mikono ya wanawake ya Business Times Limited, leo imeibika washindi wa kombe la NSSF 2014 baada ya kuibuka kidedea kwa kuichapa timu ya Zanzibar mabao 26 - 13 katika mchezo uliochezwa jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC, Chang'ombe. Upande wa wanaume nao waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Changamoto, 3 - 0 na kutwaa kombe la NSSF 2014

Chini: Kilia mwenye kofia ni Mhariri Mtendaji wa Majira, Imma Mbuguni akipokea kombe la ushindi wa wanawake baada ya timu ya Business Times Limited kutwaa ubingwa wa kombe la NSSF leo katika fainali iliyochezwa katika viwanja vya TCC, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.





No comments:

Post a Comment