Thursday, April 24, 2014

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA MIKIA 20 YA TEMBO

Tunduru

Iddi kihambwe Ndomondo (30) wa Kijiji cha silabu Wilayani Masasi Mkoani Mtwara amefikisha katika mahakama ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tunduru ili kujibu Shauri la Uhujumu Uchumi linalo mkabili.

Akimsomea shtaka hilo kesi namba CC 30/2014  mbele ya hakimu wa mahakama hiyo felix Nyalanda, mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa polisi Inspekta Songelaeli Jwagu alisema kuwa mtuhumiwa huyo alinaswa akiwa na mikia ya Tembo 20.

Inspekita Jwagu aliendelea kufafanua kuwa katika tukio hilo mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha vifungu vya sharia namba 86 kifungu kidogo cha (1) na (2c) na namba II vya sharia  namba 5 ya uhifadhi wa Wanyama namba 5 ya mwaka 2009 ikisomwa pamoja na aya ya 14 D cha jedwali la kwanza sehemu ya 57 (1) na (2) vya sharia ya kudhibiti uhujumu uchumi sura ya 200 kama kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


Alisema katika Tukio hilo mtuhumiwa huyo alinaswa na Polisi April 21, 2014 majira ya saa 3.00 asubuhi katika eneo la Biasi Mjini hapa akiwa na mikia ya Tembo 20 yenye dhamani ya Shilingi milioni 480.


Mtuhumiwa huyo alikana kufanya kosa hilo, amepelekwa mahabusu ya gereza la Wilaya ya Tunduru baada ya kukosa mtu wa kumdhamini. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika kesi italekwa tena may 5 mwaka huu katika mahakama hiyo kwa ajili ya kutanjwa.


No comments:

Post a Comment