Dar es Salaam,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea amri
ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata sh. milioni 106 za Klabu ya Yanga
kutokana na mapato ya milangoni kwenye mechi zake, ili kuwalipa waliokuwa
wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ofisa
Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema tayari wameanza utekelezaji wa amri
hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Rhino Rangers
iliyochezwa Machi 22, mwaka huu mjini Tabora wamezuia sh. 9,221,250 ambazo
ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh.
38,655,000.
SOMA ZAIDI. . .
SOMA ZAIDI. . .
Alisema wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga
mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi
na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni
106.
"Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu,
vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba
wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa
wengine," alisema Wambura.
Alisema iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira, wafuate
taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande
mmoja unataka kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment