Sunday, March 30, 2014

WANAKIMBIJI: JESHI LINATUNYANYASA, TUNAISHI KWA MASHAKA

File photo
Uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na kikosi kimoja cha jeshi la wananchi JWTZ unazidi kuwa kero wananchi wa maeneo ya Kimbiji, Wilaya ya Temeke, Dar-es-salaam.  Kutokana na kuvamiwa na wanajeshi katika makazi na maeneo yao ya ardhi, ambapo wanajeshi wanawalazimisha wananchi waondoke bila ya ridhaa yao, wala kufuata misingi na taratibu za sheria za ardhi ya raia hao na kuwapa usumbufu familia za raia hao wakiwemo akina mama na watoto.

Pamoja na wananchi wa Kimbiji kulalamika mara nyingi katika vyombo vya habari, pia katika vyombo serikali kuhusu majanga haya, cha kusikitisha hakuna jibu lolote walilo pewa. Wananchi wa Kimbiji wanasikitishwa sana na usumbufu wanao upata kutoka kwa wanajeshi JWTZ ambao wanadhamana ya kulinda nchi sio kuwanyanyasa wananchi bila ya kufuata misingi ya sheria za miliki ardhi wakati serekali nayo haijatoa tamko lolote kuhusu unyanyaswaji huo. 

Kushiriki katika kikako chochote kile kinachohusu kugawa maeneo au kupisha mradi wowote ule wa maendeleo na Jeshi JWTZ. Wananchi wa Kimbiji wamedai kuwa wanajeshi wana lengo la kuwapora Ardhi kwa kutumia vitisho vya kofia na nembo ya JWTZ.

IMETUMWA NA 

WANANCHI WA KIMBIJI


No comments:

Post a Comment