TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la
Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha
Muungano Wetu Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake.
Kongamano hili la Vijana kuhusu Muungano
linafanyika Jumapili Machi 30, 2014
kuanzia Saa 5:00 Asubuhi katika
ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja na
Televisheni ya Taifa, TBC One na TBC Taifa.
Kongamano hili ni sehemu ya sherehe za miaka
50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu kuasisiwa kwake na Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa
Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Aprili 26, 1964.
Kauli mbiu ya sherehe za Miaka 50 ya
Muungano ni “UTANZANIA WETU NI MUUNGANO
WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA”.
Lengo la Kongamano hili ni kuzungumzia
Wajibu wa Vijana katika kuimarisha Muungano ambao mwezi ujao unafikisha
miaka 50.
Washiriki wa Kongamano hili ni vijana 300 kutoka Vyuo vya Elimu ya
Juu vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Washiriki wa Kongamano hili watapata
fursa ya kuwasikia watoa mada ambao ni Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Prof. Gaudens Mpangala atakayewasilisha
mada kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano, Miaka 50 tangu
kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha mada kuhusu Mapendekezo
ya Katiba Mpya kwa Mustakabali wa Muungano wetu itawasilishwa na Prof. Issa Shivji.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali
mbali vya Habari nchini wanakaribishwa kushiriki kwa lengo la kuhabarisha umma
kuhusu kongamano hili.
Imetolewa
na Idara ya Habari - MAELEZO
29 Machi
2014
No comments:
Post a Comment