Sunday, March 23, 2014

MTOTO WA MIAKA 14 ALAWITI MTOTO WA MIAKA 2, ASHIKILIWA POLISI


Moshi

Mtoto Elias Ndamka mwenye umri wa mika 14 anayesoma shule ya msingi Kaloleni anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kmlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 2 na kumuumiza vibaya.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alisema tukio hilo lilitokea juzi(Machi 20 mwaka huu) majira ya saa saba mchana katika kata ya Kaloleni manispaa ya moshi. Alisema siku ya tukio wazazi wa watoto hao hawakuwepo nyumbani na kuwa kutokana na nyumba zao kuwa jirani Ndamka alimwita motto huyo na kumuingiza katika nyumba yao na kumfanyia kitendo hicho.

"Nyumba za watoto hawa ni jirani sana hivyo wazazi wa mtoto huyu wa miaka miwili alidai kuwa alitoka kidogo ambapo aliporudi akawa anamtafuta mwanaye na kumkuta akiwa na kijana huyo tayari akiwa amelawitiwa"alisema.

Alisema mwanafunzi huyo (Ndamka) anayesoma darasa la saba katika shule ya Kaloleni bado anashikiliwa na jeshi la polisi ili uchunguzi kuendelea na kuwa mtoto huyo anatibiwa katika hospitali ya mkoa Mawenzi. Aidha kutokana na matukio hayo kamanda Boaz ameonya tabia ya baadhi ya watu wenye mabanda ya video kuonyesha picha zisizostahili kwa watoto jambo linalopelekea kuongezeka kwa matukio hayo.

"Haya matukio yanafanywa na watoto nah ii inatokana na watu wasiokuwa na nia njema kuanzisha mabanda kwa madai ya kuonyesha mpira lakini wamekuwa wakionyesha watoto picha zisizofaa"alisema kamanda

No comments:

Post a Comment