Thursday, February 20, 2014

KENYA YAANZISHA USHURU WA KUKU,KUCHINJA, KUAGA MAITI, N.K

Katika Kaunti ya Kiambu, inayoongozwa na Gavana William Kabogo, kuna ushuru mpya unaotozwa kwa familia iliyopoteza mpendwa ama wapendwa wao. Ushuru huo ambao ni matokeo ya katiba ya Kenya kushusha madaraka kwa wananchi, pia hutoweza kuchinja mifugo wako nyumbani bila kulipa ushuru!

Katika Kaunti ya Kakamega, Gavana amebuni ushuru wa kuku ambapo kila mfugaji atalipa Sh20 kwa kila kuku anayemfuga. Pia, watu wanapoomboleza, lazima walipe ushuru wa kuomboleza haswa wanapotazama mwili wa marehemu.
Ukiutazama zaidi ya mara mbili, utalipa ushuru zaidi ya mara moja! Watu hawajui la kufanya na wana majuto makuu kwa kukaribisha Katiba mpya 2010. Walipokuwa wanaipitisha walikuwa na matumaini kwamba ingebadilisha maisha yao kwa kuleta utawala na huduma za Serikali Kuu karibu yao.

Wakati huo wa mchakato wa Katiba mpya, Makamu wa Rais William Ruto alikuwa katika upande uliokuwa ukipinga Katiba hiyo. Hata hivyo, Muungano wa Jubilee ulipochukua hatamu ya uongozi, Ruto na Uhuru Kenyatta waliapa kuilinda na kuitetea Katiba hiyo. (Mwananchi)


No comments:

Post a Comment