Timu za Uingereza zimezidi kuandikisha matokeo mabaya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal ilipigwa mabao mawili kwa bila na Beyern Munich ya Ujerumani katika mchuano wa robo fainali. Arsenal ililazimika kuwachezesha wachezaji kumi pekee uwanjani baada ya mlinda lango wake kuonyeshwa kadi nyekundu.
Mchezaji Mesut Ozil alipoteza penalti ya Arsenal katika kipindi cha kwanza sawa na David Alaba aliyeshindwa kufunga penalti ya Bayern Munich.
Hii inatokea baada ya Manchester City kuchapwa mabao mawili kwa bila Jumanne na Bercalona ya Uhispania. Timu nyingine za Uingereza ambazo ziko katika kinyang'anyiro hicho ni Chesea na Manchester United ambazo zitacheza michuano hiyo baadaye mwezi ujao.
Katika mechi nyingine iliyochezwa hapo jana Atletico Madrid ya Uhispania iliishinda AC Millan ya Italia bao moja kwa bila na ikiwa itasonga mbele hii itakuwa mara ya kwanza Atletico Madrid kuingia robo fainali tangu mwaka 1997. (BBC)
No comments:
Post a Comment