Thursday, February 13, 2014

URAIS 2015, VIGOGO 3 CCM WAWEKWA KITIMOTO, WENGINE KESHO


Kamati ndogo ya maadili ya CCM imekutana Dodoma na kuwahoji wanachama watatu wa chama hicho wanaodaiwa kutangaza nia ya kugombea Urais na kuanza Kampeni za Uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kinyume na utaratibu na maadili ya chama hicho.

Kamati hiyo inayoongoza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama, Abdurahman Kinana ,wajumbe William Lukuvi,Maua Daftari,Pindi Chana mtu wa kwanza kumhoji alikuwa ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa aliehojiwa kwa saa moja na Nusu ,na baadaye aliongea na waandishi wa habari.

Na wengine waliohojiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Wiliam Ngereja ambao hawakuwa tayari kuzungumza na waandishi na kusema kamati hiyo ndiyo yenye jibu sahihi


Baada ya zoezi hilo kukamamilka waandishi wa habari walitaka kupata ufafanuzi zaidi wa mahojiano hayo kwa katibu mkuu wa chama hicho Abdurahaman kinana,yeye hakuwa tayari kuzungumza licha ya kusema kuwa kamati hiyo itaendelea kuwahoji viongozi wengine hapo kesho.


Miongoni mwa wale watakaohojiwa kesho ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na uratibu Steven Wassira,Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe,pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba.

No comments:

Post a Comment