Dkt. Julius Nyang'oro akitoka mahakamni akiambatana na mkewe (wame shikana mikono, na mwanasheria aliyetangulia mbele huku wakizongwa na waandishi wa habari.(picha kwa hisani ya mtandao) |
HILLSBOROUGH, Marekani
Mhadhiri wa zamani mwenye kashfa inayohusisha wachezaji
kwenye Chuo Kikuu cha North Carolina (UNC), kitengo cha Chapel Hill, Julius
Nyang'oro (Pichani Kulia), amefunguliwa mashitaka, akituhumiwa kupokea dola za Marekani 12,000
yakiwa malipo ya mafundisho huku hakuwa na darasa lolote la kufundisha.
Prof. Nyang'Oro alikuwa mwenyekiti wa Kitengo cha Masomo
ya Afrika na yale ya Marekani yenye asili ya Afrika kwenye Chuo Kikuu hicho.
Mwanasheria wake,
Bill Thomas, alisema mapema wiki hii kwamba mteja wake anakusudia
kupigana na kesi ya udanganyifi wa kimasomo iliyofunguliwa dhidi yake.
Dkt. Nyang'oro bado anachukuliwa hana makosa chini ya
sheria yetu,ö Bw. Thomas, mwanasheria wa
Durham, alisema.
Kumekuwepo na upande mmoja wa kisa hiki ambacho
kimewekwa kwenye vyombo vya habari, lakini atapata fursa ya kuwakilisha utetezi
wake. Tunakusudia kuiwakilisha kesi yake mahakamani. Atapigana na mashitaka
yaliyofunguliwa dhidi yake,ö alisema mwanasheria huyo.
Hata hivyo, Bw. Nyang'oro alijiuzulu uenyekiti 2011
wakati wa uchunguzi kwenye chuo hicho ambao uligundua baadhi ya madarasa katika
kitengo hicho walimu walikuwa hawafundishi, mabadiliko ya kiwango yasiyowekewa
kumbukumbu na saini batili za kitengo kuhusu taarifa za viwango.
SOMA ZAIDI...
Akipatikana na hatia, Bw. Nyang'Oro anaweza kutumikia
kifungo gerezani cha miezi 10. Hata hivyo, uongozi wa chuo ulisema ulizipata
dola hizo 12,000 kutoka katika hundi ya mwisho ya malipo kwa Bw. Nyang'Oro.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani la
'Associated Press, mwanasheria wa Jimbo la Orange, James Woodall, alisema Prof.
Nyang'Oro alipaswa kutoa mihadhara darasani ya mara kwa mara majira ya joto kwa
mwaka 2011.
Lakini, Bw. Woodall alisema badala yake Prof. Nyang'oro
alikuwa akitoa mhadhara huru wa masomo ambao ulihitaji wanafunzi kuandika
mitihani ambayo haikufanywa.
Chuo pia kiligundua kwamba kozi hiyo iliyokuwa ikitolewa
na Prof. Nyang'oro, ambayo ilikuwa nyongeza ya mwisho katika ratiba ya masomo,
ilikuwa ikihudhuriwa na wachezaji 18 wa mpira wa miguu na mchezaji wa zamani wa
mchezo huo.
Taarifa ya uchunguzi wa chuo kuhusu kashfa ya udanganyifu
wa masomo iliyotolewa mwaka jana ilimlenga Prof. Nyang'oro na afisa utawala wa
idara ambaye pia amejiuzulu wadhifa wake.
Timu ya uchunguzi iliyoongozwa na Gavana wa zamani, Jim
Martin, ilihitimisha kwamba udanganyifu huo haukuhusisha kitengo kingine au
watu wengine wa idara ya michezo.
Martin, mhadhiri wa zamani wa kemia wa chuo hicho,
alisaidiwa na washauri wenye uzoefu katika uchunguzi wa kimasomo.
Baada ya mapungufu ya mbinu iliyotumika ya ripoti hiyo
kujulikana, Martin na maafisa wa chuo hicho walisema walikosa nguvu za hati za
Kitengo cha Upelelezi cha Jimbo (State Bureau of Investigation, au SBI),
kuwalazimisha watu kujibu maswali na kutoa ushahidi.
"Chuo hicho na Bw. Woodall waliitegemea SBI kusaidia
kujua kama matendo yoyote ya uhalifu yalikuwa yametokea, kwani SBI ilikuwa na
nguvu pana za kiuchunguzi ambazo chuo kilizikosa," alisema Bw. Tom Ross,
rais wa mfumo katika Chuo Kikuu cha Jimbo.
Bw. Ross aliongeza kusema katika taarifa yake Jumatatu
kwamba ushirikiano unaoendelea wa chuo wenye mchakato wa kiuhalifu utaendelea
katika hitimisho lake.
Bw. Martin alisema kulikuwa hakuna ushahidi kwamba idara
ya michezo ya chuo iliwalazimisha wanafunzi kuchukua kozi zenye taratibu
zisizoeleweka ambazo zingewafanya wanamichezo kustahili kushiriki mashindano.
No comments:
Post a Comment