Monday, February 24, 2014

AVUA NGUO YAKE YA NDANI NA KUFANYA VITUKO HADHARANI

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida, watu walipigwa na butwaa katika msiba wa muendesha magari maarufu nchini Afrka Kusini, Bongani Makhubo (40).

Katika msiba huo waendesha magari waliamua kupiga misele, wakati magari yanaendelea kufanya vitu vyao, msichana mmoja aliingia katikati ya misele hiyo na kuvua nguo yake ya ndani kisha kuanza kucheza muziki.

Lakini sio kila mtu alifurahishwa kuona akipepea nguo yake ya ndani hewani, alieleza john Lelaka akidai “watu wanaruhusiwa kushangilia lakini sio kwa namna ambayo inawasumbua wengine.”

Baada ya mazishi ya Bongani, waendesha magari walifanya mashindano ya magari ambapo zaidi ya magari 300 yaliingia na kuanza kupiga misele.

No comments:

Post a Comment