Friday, February 21, 2014

AJALI MBAYA, WATU WOTE WATEKETEA NA KUBAKI MAJIVU

Ajali mbaya iliyotokea jumatano saa 07:40 mchana, iliyohusisha lori la kampuni la East African Company yenye namba za usajili T340AWW, aina ya Scania Tanker iliyokuwa na tela ya mafuta yenye usajili namba T790ABH ilipinduka baada ya kuacha njia na kuteketea kwa moto (TAZAMA PICHA).

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la mlima Sekenke wakati gari hilo likiwa linatokea Singida kuelekea Igunga mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi mkoani Singida, gari hilo likiwa limebeba mafuta ya Petrol lilipofika eneo halo la mlima Sekenke liliacha njia na kuingia kwenye mtaro kando ya barabara na kulipuka kwa moto ambao chanzo chake hakikuweza kufahamika mara moja.





Walioshuhudia wa ajali hiyo wanasema moto huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kuunguza gari lote na watu wote wliokuwemo ndani ya gari hilo.

ANGALIA PICHA, SOMA  ZAIDI…

Inadaiwa kulikuwa na watu watatu na wote walipoteza maisha papo hapo kutokana na moto huo. Dereva wa gari hilo ni miongoni mwa watu walipoteza maisha kwenye ajali hiyo. Dereva huyo alitambuliwa kwa jina la OSWARD PETER ama kwa jina maarufu MPANDA inakadiriwa kuwa ana umri wa miaka 33.

Wengine waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni utingo wa gari hilo aliyetambulika kwa jina moja tu la YUSUPH na mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la SALMA JUMANNE mabaye anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30.
Haikuwa rahisi kupatikana kwa nyaraka zozote muhimu kwenye ajali hiyo kutokana na ukweli kwamba kila kitu kiliungua moto


No comments:

Post a Comment