Wednesday, January 22, 2014

UGOMVI WA VIJIJI, AUAWA KWA PANGA, 17 WAJERUHIWA VIBAYA

Singida

Mtu moja mkazi wa Kijiji cha Nduamghanga Tarafa ya Mgori Wilaya ya Singida vijijini Athuman Jumanne (40) ameuawa kwa kukatwa panga kichwani na kuchomwa mshale na wengine 17 kujeruhiwa baada ya watu waliotoka kijiji jirani kuvamia eneo hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Geofrey Kamwela chanzo cha mauaji hayo yaliyofanyika tarehe 21 mwezi huu saa 7:30 mchana ni ugomvi uliyozuka kati ya watu hao na wakazi wa kijiji cha Nduamghanga waliosadikiwa kutoka kijiji cha Handa wilayani Nchemba Mkoa wa Dodoma.

“Ugomvi huo ulizuka siku hiyo baada ya watu hao wasiyojulikana idadi yao na wanakijiji cha Nduamghanga wakidai kurejeshewa ng’ombe 180 waliyokamatwa baada ya kuingia kwenye hifadhi yam situ wa asili wa Mgori mnamo 20/01/2014”. Alisema Kamwela.

Alisema katika ugomvi huo marehemu ambaye alikuwa mkatapori wa kijiji hicho (VGS) alishambuliwa kwa panga na mishale na kufariki dunia papo hapo huku wengine 17 walijeruhiwa na moja vibaya.

Aliwataja waliyojeruhiwa kuwa ni pamoja na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Mwafutari Rajabu (35) Elisante Saidi (51) aliyejeruhiwa kwa panga na mkuki sehemu za kichwa, mikono yote miwili kifuani na paja la kulia ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa ajili ya matibabu.

Alisema wengine ambao walitibiwa katika Zahanati ya Nduamghanga kuwa ni Hamisi Ramadhani (36) Omari Omari (42) Muna Hamisi (38) Abraham Mohamed (60) Hamis Rajabu (33) Yohana Said (37) Ramadhani Rajabu (26), Msafiri Juma, Omari Hamis (33) Hamisi Sharifu (32) Jumanne Hassani na Abeli Muna.



Kamanda huyo wa Polisi aliongeza kuwa mwingine ni Daudi Karata (71) ambaye licha ya kuvamiwa na kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake, pia alinyang’anywa bunduki yake ya aina ya SHORT GUN na risasi zake nne na watu hao kutoroka nayo kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment