Sunday, November 02, 2014

AJALI MBAYA BAGAMOYO, YAHUSISHA ALTEZZA, DEREVA ALIKUWA CHAKARI

Ajali mbaya imetokea leo wakati dereva wa gari dogo Toyota Altezza yenye usajili namba T786DBP (PICHANI),  alijaribu kulipita lori la mafuta na alipokutana uso kwa uso na pikipiki kisha kuigonga na kusababisha lifo cha dereva wa bodaboda, kisha kuserereka na kutumbukia bounden. 
Dereva wa gari dogo amejeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika taya na kung'oka meno yote. Imedaiwa kuwa baada ya kupekua gari lake yalikutwa makopo 8 ya pombe aina ya Castle Lager yakiwa yameshatumika( kunywewa). 

Ajali hiyo ilitokea Bagamoyo eneo la katika ya Zinga kwa Mtoro na Shamba la Minazi la Chambezi katika barabara kuu ya Bagamoyo -Dar.
Picha zone kwa hisani ya SALUM ALLY






No comments:

Post a Comment