Saturday, January 04, 2014

TAARIFA KUHUSU SHIRIKA LA RELI TANZANIA

                                                        KAMPUNI YA RELI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI YA
ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JANUARI 05, 2014




Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014 saa 3 usiku imeahirishwa hadi kesho Jumapili Januari 05 , 2014, saa 3 usiku.

Taarifa imefafanua kuwa kutokana na mvua kunyesha mkoani Dodoma na mikoa jirani eneo kati ya stesheni za reli ya kati za Gulwe na Godegode zimejaa maji na kufunika njia ya reli mkesha wa mwaka mpya wa 2014!.

Tokea juzi Januari 02, 2014 Wahandisi na mafundi wa kampuni za TRL na Rahco kwenye sehemu husika wakifanya tathmini na kusimamia ukarabati wa maeneo mawili ya reli yaliyoharibika.

Kwa mujibu Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu anayeongozwa kikosi kazi cha kukarabati amesema kazi ya ukarabati inafanywa usiku na mchana kuona huduma zinaanza mapema iwezekanavyo ikiwemo huduma ya usafiri wa treni za abiria uliopangwa kuanza tena hapo kesho Jumapili Januari 05, 2014.

Kutokana na dharura hii treni za kutoka Mpanda, Kigoma na Mwanza kuja Dar zimebadilishiwa muda na siku ya kuondoka hivyo basi, badala ya kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014 sasa zitaondoka kesho Jumapili Januari 05, 2014 saa 2 asubuhi.

Aidha taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.

TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 04, 2014

No comments:

Post a Comment