Sunday, January 05, 2014

NMB SIJUI KAMA HII MMEIONA AU KUISIKIA...

Njombe

Wateja wa benki ya NMB katika halmashauri ya Mji Makambako wameitaka benki hiyo kuboresha huduma ili kuweza kumudu ushindani uliopo katika asasi za kifedha.

Hayo yametolewa na wadau wa benki hiyo wakati wa hafra fupi ndani ya ukumbi wa Durban hotel ikiwa ni mipango itakayotekelezwa ndani ya 2014, iliyoandaliwa na NMB Tawi la Makambako.

Wadau waliopata fursa ya kuhudhuria hafra hiyo wametoa maoni mbalimbali katika dhana nzima ya huduma zinazotolewa katika benki hiyo, kwamba pamoja na kuwepo kwa changamoto za utoaji huduma kwa ,wateja,kupunguza msongamano wa foleni.

Katika suala la utoaji mikopo hususani kwa watumishi wa serikali Kwa niaba ya wadau hao Fidelis Maona alishauri alishauri
mikopo inayotolewa kwa watumishi isisubiri kumalizika kwa mkataba badala yake mteja aruhusiwe kumaliza mkopo mapema kulingana na uweo wake ili kumpa fursa kukopa tena.

Upande wake John Mwandoloma alisema, idadi kubwa ya wateja ni dalili tosha kwamba benki hiyo imezidiwa na kuwataka viongozi kulifanyia kazi suala la mrundikano wa wateja wa nje na ndani ya benki ili kuondoa hali ya kupoteza muda kwa wananchi ambao wanategemea kupata huduma na kujikuta wanapoteza muda mwingi wakisubiri.

Meneja wa benki hiyo Mica Mwakila amesema utoaji mikopo unafuata kanuni na sheria zil;izoweka kinyume na hapo ni ukiukwaji wa taratibu za kibenki hata hivyo amesema hafla hiyo ni mkakati wa kuboresha huduma na kuwapa fulsa ya kutambua mahitaji ya wateja wao.

Alisema, kutokana na wateja wa NMB kuwa ni wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, benki hiyo inatarajia kuanza kutoa VISA Card kwa wateja wake yote ikiwa ni kuhakikisha wateja wanafanya biashara na benki hiyo kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment