Tuesday, January 28, 2014

MVUTA SIGARA MAARUFU DAUNIANI WA MARLBORO AMEFARIKI

Mtu pekee aliyeweza kuibadilisha na kuinua mafanikio ya sigara duniani haswa sigara maarufu ya Marlboro, Eric Lawson (Pichani kulia) amefariki dunia.

Mwanaume aliyekuwa na mvuto, mcheza filamu ambaye alikuwa mpanda farasi maarufu Southwest, aliyetoka Texas mpaka Colorado na kwenda Arizona nchini Marekani, ambaye pia aliweza kuinua kampuni ya Phillip Morris Tobacco na kulinda utamaduni wa kweli wa Kimarekani wa Cowboy, na kweli aliweza kuvuta sigara za Marlboro mpaka paketi 3 kwa siku.

Lawson alikuwa bado anavuta sigara mwaka 2006 alipogundulika kuwa na ugonjwa usiotibika wa mapafu. Alifariki dunia kutokana na ugonjwa huo akiwa nyumbani kwake San Luis Obispo tarehe 10 mwezi januari akiwa na miaka 72.

Kwa miaka 3, mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni wa miaka ya 80, Lawson alipata umaarufu mkubwa katika matangazo na kuwakilisha utamaduni wa kimarekani.

Katika miaka kadhaa iliyopita Lawson aliongelea sana na kwa ukali madhara ya uvutaji sigara, alifanya huduma za kujitolea na kutoa matangazo kadhaa kwaajili ya taasisi ya saratani ya Marekani ya American Cancer Society miaka ya 90, ikiwa ni miaka michache kabla hajaacha kuvuta sigara.

“Alijitahidi kuongea na watoto, kuwaambia wasianze kuvuta sigara”, alisema mkewe Susan Lawson akiliambia shirika la AP akiongeza “alijua sigara ilichomfanya”

No comments:

Post a Comment