Tuesday, January 28, 2014

WAZIRI MUHONGO AWEKA SAINI LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI

DSM,

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo(Pichani anaye saini)   ameweka saini Leseni tatu za Uchimbaji wa Madini kwa Kampuni zinazotarajia kuzalisha madini aina mbalimbali kulingana na maeneo waliyoomba kufanya shughuli hizo.
Kampuni zilizosainiwa Leseni ni Kampuni ya J.S Construction, inayomilikiwa na Bw. Sisti Slyvester Mganga ambaye ameingia ubia Bw. Nakui Chen Kampuni hiyo yenye Leseni ML 501/2014 ina eneo la ukubwa wa km 0.29. Aidha, shughuli za uchimbaji zitafanyika katika eneo la Kihangaiko Bagamoyo na Madini yatakayozalishwa ni ‘dimension stone’ na kokoto za ujenzi za granite.

Vilevile, kampuni nyingine iliyowekewa saini ya Leseni ni Osiris Gold (T) Ltd. inayomilikiwa na Watanzania Ezekieli Kihali na Shehdaza Walli leseni namba ML 513/2014. Madini yatakayozalishwa na Kampuni hii ni dhahabu katika eneo la ukubwa wa km 9.94, Rwamgaza Geita

Aidha, Mhe. Muhongo ameweka saini leseni ya uchimbaji wa madini aina ya Marble kwa Gagan S.Gupta, Sameer S.Gupta na Shailesh B.Bhandari ambao wanamiliki Kampuni ya Kamal Steel katika eneo la Kidayi Kilosa. Kampuni hii yenye Leseni ML 514/2014 ina eneo la Km 9.52.

Wakati akitoa Leseni hizo za uchimbaji, amewakumbusha wamiliki wa leseni kuhusu kodi na wajibu wa mwenye leseni katika jamii inayohusika ili wananchi na Taifa waweze kufaidika na rasilimali hizo. Uwekaji saini huo umefanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, Dare s Salaam.





No comments:

Post a Comment