Friday, January 24, 2014

HALI BADO MBAYA DUMILA, MAGUFULI AENDA KUSAIDIA


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka eneo la tukio, hali bado tete kama inavyoonekana kwenye picha. Waziri wa ujenzi DR. John Pombe Magufuli yupo hapa Morogoro kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa barabara inayotumika kwa sasa.

Magari makubwa yaliyobeba mafuta na mizigo yamepaki ktk eneo la Dakawa, Magole na mizani Mkundi, kwa sasa kuna wachina wanaleta mawe kwa ajili ya matengenezo ya awali, na kuna vijana wanafanyakazi ya kutoa matope.

Magari makubwa ya kubeba mafuta na mizigo hayawezi kupita kwenye njia inayotumika kwa sasa kutokana na barabara kuwa nyembamba, Magari yanayoruhusiwa ni magari ya tani 12 tu.


No comments:

Post a Comment