Tuesday, December 24, 2013

MADEE, CHEGE KUWASHA MOTO COCO BEACH XMASS DAY

 Katika kuhakikisha sikukuu za krismas inaenda vyema, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imeandaa Tamasha kwa wateja na mashabiki wa Muiki katika viwanja vya fukwe za Coco wakati huu ikiwaleta wasanii ambao wako juu kimuziki Madee(Kulia chini) na Chege(kushoto chini).

Wasanii hao watatoa burudani bure kwa wakazi wa Dar wote watakao jitokeza katika viwanja hivyo huku pamoja na mambo mengine watashuhudia simu za kisasa za Huawei zikiuzwa katika wakati huo wa Burudani.

Tamasha hilo litafanyika kwa siku tatu yaani krismas yenyewe yaani tarehe 25 na, 26 maarufu kama Boxing Day pamoja na mwaka mpya ambao litawawezesha wateja kujinunulia simu za kisasa kwa bei nafuu ambazo zitakuwa zimeunganishwa moja kwa moja na vifurushi vyenye nguvu vya intaneti vya mtandao huo.

Akizungumza na chombo hichi cha Habari Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa amesema wameona si kitu kizuri kumaliza mwaka hususani katika kipindi hiki muhimu cha sikukuu na kuukaribisha mwaka mpya bila ya kuwapatia kitu chochote cha kusindikiza shamrashamra hizi za sikukuu wateja wao.

“Vodacom kwa kushirikiana na Huawei ambao mbali kuwa na bidhaa mbalimbali za umeme pia wanasimu za kisasa kabisa zenye program zote muhimu ambazo watu wanazitumia na kuzipenda kama vile Facebook, Twitter, Whatsup, Viber, Skype na pia uwezo wa kuperuzi Mtandao yote ya kijamii”blogs” na wavuti mbalimbali ambapo tutawawezesha kwa intaneti ya mtandao wetu wenye nguvu bila kikomo.” Alisema Twissa na kuongeza.

“Tunatambua mchango mkubwa wa wateja wetu ambao wamekua wakitunga mkono kila siku hivyo Tamasha hili ni maalum kwa ajili yao “Hivyo basi hii ni fursa ya kipekee kwa wateja wetu, naweza sema hii ni zawadi ya krismas na mwaka mpya, nawaomba wachangamkie fursa hii.”

Twisa aliongezea kuwa “mbali na kujinunulia simu hizo pia kutachezeshwa droo ya bahati ambapo washindi watapatikana papo kwa papo, pia kutakuwepo na wasanii lukuki wa bongo flava ambao watapamba jukwaa la Vodacom krismas Bonanza.
“Siku ya krismas Mzee wa nani kamwaga pombe yangu na tema mate tuwachape, Madee au Rais wa Manzese na Wakali Dancers watatoa burudani ya kufa mtu kwa wakazi watakaojitokeza siku hiyo pia siku ya Boxing Day ni zamu ya mkali wa TMK Wanaume, Chege Chigunda, Mtoto wa Mama Said au Mvunja nazi kwa Ugoko, kuwapeleka mashabiki uswazi Take away huku mchawi wa jukwaani katika historia ya muziki wa bongo flava Tanzania kutoka TMK Wanaume Halisi, Juma Kassim Abdallah Kiroboto ‘Nature’ a.k.a Kibra atafunga kazi kwa shoo ya kufa mtu na kuwakaribisha watanzania siku ya mwaka mpya wa 2014.” Alisema Twissa.

“Hii si ya kukosa, ningependa kuchukua fursa hii kuwataka wateja wetu na watanzania kwa ujumla waje Coco beach siku hizo za bonanza na kufurahi kwa pamoja mafanikio haya ambayo kwa kiasi kikubwa ni jitihada zetu kuwahudumia ipasavyo na kutuunga mkono kwenu, hivyo hatuna budi kuwaandalia tukio ambalo litawafanya wafurahi na marafiki zao na kuwafanya wapate sehemu yakutembea na sio kubaki ndani hasa katika msimu huu wa siku kuu” Alimalizia bosi huyo wa Masoko wa Vodacom.
Kwa upande wake Meneja Masoko na usambazaji wa Huawei Technogies Tanzania,Ramadhan Nkanyemka amesema simu hizi ni za kisasa na bora kukidhi mahitaji ya watumiaji tena zinapatikana kwa bei nafuu tu.

“Huawei kushirikiana na Vodacom ni jambo la kujivunia kutokana na jinsi huduma na bidhaa zake zilivyotapakaa kila mahali, nawataka wateja wetu kufika kwenye maduka ya Vodacom na Huawei kujipatia simu za kisasa kabisa ambazo zitawawezesha kuwa katika ulimwengu wa digitali ambao kila kitu kinapatikana kwenye intaneti.” Alisema Nkanyemka.Na kuongezea “Mteja pindi anunuapo bidhaa zetu atawezeshwa kwa vifurushi vya intaneti kutoka mtandao huu wenye kasi na ulioenea nchi nzima.

Simu ambazo zitauzwa katika maduka ya Vodacom na ya Huawei ni pamoja na Huawei Y210D, itakayouzwa kwa 162,000, Huawei W1 itakayouzwa kwa 360,000, Huawei G510, 350,000 , Huawei Ascend W1 360,000, Simu nyingine zitakazo kuwa na GB 5 za internet ni Huawei Ascend P6 itakayouzwa 800,000 na Huawei Ascend Mate kwa shilingi 900,000.


No comments:

Post a Comment