Wednesday, November 06, 2013

MKIMBIAJI WA MIAKA 86 AFARIKI BAADA YA KUMALIZA MBIO

Mkimbiaji mwenye umri wa miaka 86 amefariki baada ya kumaliza mbio hizo juzi (jumatatu) katika mbio za nyika za 25 za New York (25th New York City Race). 

Joy Jonhnson (Pichani chini kulia) mwanamke kutoka San Jose, nchini Marekani alikumbwa na mauti siku ya jumatatu baada ya kumaliza mbio hizo na kusimama nje ya studio za TODAY na kuongea na msoma taarifa ya hali ya hewa Al Roker wa Wall Street Journal.

Kwa mujibu wa bintiye, Bi Johnson alizimia baada ya kumaliza maili 16 siku ya jumapili ambapo alikataa ushauri wa kwenda hospitali na kuamua kumalizia mbio hizo ambapo alitumia masaa 7 dakika 57 na sekunde 41.

Inadaiwa Bi Johnson alianza mazoezi ya kukimbia mwaka 1985, ambapo alikimbia kila siku kwa masaa mawili.





No comments:

Post a Comment