Monday, November 04, 2013


MENGI AMTOLEA UVIVU MUHONGO KATIKA TWITTER

Kuhusu Mh Muhongo kusema hatuna fedha, akumbuke dunia ya leo hufanyi biashara na fedha ulizonazo mfukoni bali maarifa uliyonayo kichwani




Watu wakumbuke kwamba karibu vitalu bora vyote vya gesi vimekwishatolewa kwa wageni.




TPDC ni shirika la umma. Sisi sio waporaji wa mali ya umma. Sisi tunapigania sehemu ya kile ambacho Mh Muhongo anataka kuwapa wageni.




TPSF inataka Wazawa wapewe vitalu vya gesi kama wanavyopewa wageni na kwa kufuata Sheria namba 16 ya 2004 na Sera ya Uwezeshaji ya 2004




Mh Muhongo asema TPSF inataka kuchukua nafasi ya TPDC na hivyo kurubuni Watz. Huu ni uongo na upotoshaji wa makusudi. Aombe radhi


Kheri mwendawazimu aliyevua nguo kuliko aliyevaa maridadi. Inaweza kuchukua muda mrefu kabla hujafahamu aliyevaa maridadi ni mwendawazimu




Jamani rushwa ya Dola inaweza kukufanya kichaa. Rushwa ya pesa ya madafu si tamu na ni rahisi kujulikana


Je Mh Muhongo anataka kuwadanganya Watz kwamba wafanyabiashara wa nje ni wasafi?




Mh Muhongo asema wafanyabiashara wazawa wa Tz ni watoa rushwa. Ndio sababu ya kutowapa vitalu vya gesi. Mbona hawataji?




Mh Muhongo amewatukana wazawa wa Tz kwa kuwaita fukara na kwamba wana uwezo wa kufanya biashara ya juisi tu. Aombe radhi




Nilimwandikia Mh Muhongo kumtaka aniombe radhi kwa kunitukana. Lakini amekataa hata kujibu barua yangu






No comments:

Post a Comment