Thursday, October 10, 2013

P -SQUARE KUPAGAWISHA DAR

WASANII mapacha kutoka nchini Nigeria P -Square wanaotamba na kibao kinachojulikana 'Personally' wanatarajia kufanya shoo ya kipekee nchini Novemba 23 mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wasanii hao ambao wanaendelea kukonga nyoyo za mashabiki wao ndani ya nje ya bara la Afrika wanatarajia kufanya onesho hilo nchini huku wakisindikizwa na wasanii wakali wa hapa nyumbani.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar, Hillary Daudi wa East Afrika Radio, Amesema onesho hilo litakuwa la kipekee. P- Square wataongozana na wasanii wengine 13 ambao watatoa burudani ya Live Band siku hiyo. Pamoja na wasanii wengine kutoka Tanzania.

“Wote tunatambua namna kundi hili linavyofanya vizuri ndani na nje ya bara la Afrika, licha ya kutoa burudani kwa mashabiki, pia litatoa fursa kwa wasanii wa ndani kujifunza kutoka kwa wasanii hawa vijana ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi yao ya muziki,” alisema Daudi na kuongeza  kuwa.


“Hii itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wasanii wetu wa bongo kujifunza kwa kuangalia wenzao wanavyofanya kazi”.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho hilo  amesema Vodacom inafurahi kuendelea kuwa sehemu ya kutoa burudani kwa jamii ya Watanzania na safari hii ikiwaleta wasanii ambao ni kipenzi cha Watanzania wengi.

“Siku zote Vodacom imeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa Watanzania, kuanzia katika burudani na hata huduma nyingine za mawasiliano na kijamii. Tunaendelea kuunga jitihada za kuwainua wasanii wetu wa ndani kwa kuwapatia fursa ya kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao  wakubwa waliofanyikiwa kufanya kazi zao Kimataifa.” Alisema Twissa na kuongeza kuwa

“Kwa wateja wa Vodacom ambao pia ni mashabiki wa wasanii hawa ambao wanatamba na kibao chao kitamu cha ‘Personally’ kwa sasa wanayo fursa ya kufurahia nyimbo hizi kwa kuzidownload au kuzitumia kama miito ya simu (RBT) na kuweza kujishindia tiketi za onesho hilo"

Alitoa wito kwa Watanzania wapenda burudani kutembelea ukurasa  wa Facebook na Twitter kwa taarifa zaidi na kujua namna ya kujishindia tiketi za onesho hilo.

Tamasha hilo linaratibiwa na East Afrika Radio na TV na kudhaminiwa na kampuni ya Vodacom Tanzania Linatarajiwa kuwa la kihistoria katika burudani  ya muziki wa kizazi kipya nchini.




No comments:

Post a Comment