Thursday, October 10, 2013
DIAMOND ARUDIANA NA WEMA AU FILAMU?
IKIWA ni siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nassib Abdul 'Diamond Platnum' kukanusha vikali juu ya kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu na kumbwaga mpenzi wake wa sasa mtangazaji wa DTV Dvj Penny picha za wawili hao zaonekana wakiwa katika pozi la kimahaba.
Diamond alituma picha inayomuonesha akiwa katika pozi la kimahaba na msanii huyo Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa wawili hao wapo 'Location' kwa ajili ya kutengeneza movi aliyoandika kwa jina la 'Temptations'.
Diamond alituma picha hiyo na kuandika kuwa "katika moja ya movi ambazo naimani itakuwa ni gumzo, na mfano bora toka Tanzania hii Temptations' Star Tune soon" hayo ni maneno aliyoandika msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Istagram.
Picha hizo zimesambaa katika mitandao ya kijamii zinazoonesha wawili hao wako nje ya nchi zimezua gumzo katika mitandao hiyo huku baadhi ya mashabiki wakitaka kujua ukweli kama wawili hao wamerudiana.
Hali ya picha hizo kuzagaa kwenye mitandao imezidi kuwa gumzo ambapo mashabiki wa mwanadada Wema wamemkingia kifua na kudai kuwa watafurahi kama kweli watakuwa wamerudiana.
Hivi karibuni kuliibuka uvumi unaodai kuwa msanii huyo ameamua kurudiana na Wema huku akimbwaga Penny, ambapo mapenzi hayo yamekuwa yakiendeshwa kwa kificho.
Hali hiyo ilimpelekea Diamond kukanusha vikali uvumi huo na kudai kuwa hakuna ukweli wowote juu ya yeye kurudiana na msanii huyo.
Historia ya msanii huyo Diamond Platinum inaonesha kuwa kufanya movi na wasichana ambao mwishoni wanajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi ndio imeonekea kisingizio anachokitumia ili kufunika jambo hilo.
Inadaiwa kuwa kabla ya uhusiano wake yeye na Joketi kufahamika baadhi ya picha zilionekana na msanii huyo alidai kuwa walikuwepo kwenye moja ya kikao cha kazi, lakini ikagundulika wapo kwenye uhusiano.
Kabla ya uhusiano wake na Penny kufahamika pia kuna moja ya picha yake ilionekana wakiwa wapo chumbani wamelala na wote walidai kuwa wapo 'Location'.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment